-->

Hatimaye Alikiba Abadili Mawazo Amjibu Diamond Platnumz Kuhusu Kushiriki Wasafi Festival

GUSA HAPA CHINI KUPLAY VIDEO

Hatimaye Alikiba Abadili Mawazo Amjibu Diamond Platnumz Kuhusu Kushiriki Wasafi Festival

IKIWA ni siku mbili baada ya Staa wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wasafi Media kutangaza kuwa angetamani sana kumuona msanii mwenzake Alikiba akiungana naye kwenye Tamasha lake la Wasafi Festival, hatimaye Kiba amekubali ombi hilo na kuahidi kuwasapoti wasafi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba ameandika; “Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.
“Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi.
“Tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa. Management #RockstarAfricayangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa.
Share :
Facebook Twitter Google+

Related Posts :

 
Back To Top