
Mabeste alisema hayo baada ya kuwepo matukio mengi ya wavulana kudhalilisha wanawake waliozaa nao au waliokuwa nao likiwemo lile la muigizaji Wema Sepetu na mpenzi wake PCK.
Akizungumza na Showbiz Xtra, Mabeste alisema kuwa, vijana inabidi wajitambue na kuwaheshimu wake zao kama ambavyo wanawapenda na kuwaheshimu mama zao kwa sababu wanastahili heshima na thamani.
“Unapomdhalilisha mke wako au mwanamke wako ni sawa na umejidhalilisha mwenyewe kwa sababu mwisho wa siku nyie ni mwili mmoja, kama mnafikia uamuzi wa kuachana achaneni kwa amani sio mpaka kila mtu ajue majirani au mitandaoni,” alisema Mabeste.