Dar es Salaam. Kama wengi wataamua kufuata usemi wa “kinga ni bora
kuliko tiba”, basi waifuate huku wakichukua tahadhari dhidi ya mambo
mengine.
Lakini Rais wa Chama cha Wataalamu wa Matumizi ya Mionzi katika
Uchunguzi na Tiba (Tara), Dk Stephen Mkoloma anasema kufanya
mapenzi mara kwa mara ni moja ya njia zinazoweza kusaidia kupunguza
matatizo ya tezi dume kwa wanaume.
Hata hivyo, mtaalamu huyo anawaonya wanaume kutofanya tendo hilo
kiholela kwa sababu ya kukwepa tezi dume, akisisitiza kuwa madhara
mengine yanaweza kuwa ni kuambulia kupata magonjwa ya zinaa
ukiwamo Ukimwi.
Alisema, “Tukishauri kufanya mapenzi ya mara kwa mara fanya
nyumbani kwa mke wako, kama hauna mke basi oa na ikishindikana
Mungu ni wa rehema atatulinda kama wale wengine wasiofanya lakini
hawajapata madhara ya tezi dume.”
Akijibu maswali kutoka kwa baadhi ya wanaume waliotaka kujua ukweli
kuhusu tendo hilo kama linasaidia kuwaepusha na tezi dume baada ya
kujitokeza kupima katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Tawi la
Mloganzila, Dk Mkoloma alisema kiuhalisia kila mwanaume ana tezi
dume.
“Ili tezi dume ifanye kazi inategemea mfumo wa homoni zinazofanya
kazi sawasawa, na ili huu mfumo uwe imara unahitaji homoni ziwe
vizuri na zinakuwa vizuri baada ya kupata msisimko ambao hutokea
kwenye tendo la ndoa,” alisema.
Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu ambao hawafanyi tendo hilo
kutokana na imani au sababu nyingine, lakini hawana matatizo ya tezi
dume.
“Baada ya kuelewa hivi isije kutuondolea ile tunu yetu ya maadili, watu
waanze kurukaruka kwamba ukiona sketi unataka ooh nina tezi dume,
hapana.”
Dk Mkoloma alisema tezi dume si ugonjwa, isipokuwa ni kiungo katika
mwili wa mwanaume.
Alisema,
“Sasa katika kuishi tezi inaweza kupata matatizo kama kansa,
kuongezeka kwa ukubwa, kubadilika umbo, kwa hiyo tunachokiogopa
kwa tezi dume ni isipate ugonjwa.”
Alisema jambo la msingi ni kwa wanaume wenye umri wa kuanzia
miaka 45 kupima ili akipata majibu kuwa ana tatizo aanze matibabu
mapema.
Dk Mkoloma alisema wanaume wengi wamekuwa wakijitokeza kutibiwa
wakiwa kwenye hatua za mwisho za ugonjwa huo.
“Kwa hiyo maadhimisho haya ya siku ya wataalamu wa matumizi ya
mionzi na tiba tuliwalenga wanaume kwa sababu wanawake wanazo
kampeni nyingi,” alisema.
Hofu ya kupima
Awali, Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi Tiba, Dk Paraxeda Ogweyo
alisema wanaume wengi walikuwa wanahofia kujitokeza kupima kwa
kufikiria kuwa njia itakayotumika ni ile ya kutumia vidole kuing08/11/2018 Mtalaamu: Kufanya mapenzi mara nyingi hupunguza tatizo la tezi dume - Habari | Mwananchi sehemu za haja kubwa.
“Tuliona njia hiyo ya kuingizwa vidole itawakera watu,
tumejipanga
zaidi tunapima kwa mashine ya ‘ultra sound’, kwa hiyo wanaume
wakisikia kampeni kama hii wajitokeze,” alisema.
Dk Ogweyo alisema mwitikio wa waliojitokeza kupima ulikuwa mkubwa
na kwamba, wana imani wakitangaza tena watajitokeza wanaume wengi
zaidi.
Akielezea kampeni hiyo, mtaalamu mwingine wa radiolojia, Lulu Sakafu
alisema kansa ya tezi dume duniani ni namba mbili kwa wanaume na
tatu kwa akina baba hapa nchini.
Dk Sakafu alisema wanaume ambao katika koo zao wapo waliowahi
kupata tatizo hilo wana uwezekano mkubwa wa kuugua, hivyo ni vizuri
kupima mapema na kupata matibabu.
“Tafiti zinaonyesha sasa hivi
wanaume wa Kiafrika wanapata zaidi (tezi dume) kuliko wanaume wa
maeneo mengine (duniani),” alisema. Mbali na kupima mara kwa mara,
Dk Sakafu aliwashauri wanaume kufanya mazoezi ya mara kwa mara
pamoja na kuacha vyakula alivyovitaja kuwa ni vya ‘kisasa’.
Akizungumza baada ya kupima, Nelson Ngani alisema, “Elimu hii na
wake zetu waambiwe, kwamba tendo la ndoa ni tiba siyo tu starehe,
waache uvivu na visingizio vya mara kwa mara.”